Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara

Ada za Usajili wa Vyama/Mashirikisho na Taasisi za Michezo ni kiasi gani?

 ADA ZA USAJILI NA ADA ZA MWAKA.

Mabadiliko haya ya Ada za Usajili na Ada za Mwaka ni kwa mujibu wa Kanuni ya 25 (5) ya Kanuni za Usajili wa Vyama vya Michezo 2020.

Na.

AINA YA CHAMA

ADA YA USAJILI (Itatolewa mara moja wakati wa usajli tu)

ADA YA MWAKA (Annual fee)

1 Vyama vya Michezo vya Kitaifa vyenye wanachama wa Mikoa 200,000 150,000
2 Vyama vya Michezo vya Kitaifa Vingine 200,000 100,000
3 Vyama vya Michezo vya Mikoa 100,000 50,000
4 Vyama vya Michezo vya Wilaya 100,000 50,000
5 Vyama vya Michezo ambavyo ni Taasisi (Taasisi za Michezo) 100,000 100,000
6 Vilabu vinavyoshiriki mashindano ya Vyama vya Kitaifa 100,000 100,000
7 Vilabu vinavyoshiriki mashindano ya Vyama vya Mikoa na Wilaya 100,000 50,000
8 Wakuzaji na Wakala wa Michezo  200,000 100,000
9 Shule za Michezo (Sports academies) 100,000 100,000
10 Vituo vya Michezo (Sports Centre) 100,000 100,000
11 Vituo vya mazoezi ya Viungo (GYM & Fitness Centres) vya Kisasa 100,000 150,000
12 Vituo vya Mazoezi ya Viungo (GYM & Fitness Centres) vya kawaida 100,000 100,000

 

 

TOZO NYINGINEZO ZINAZOHUSIANA NA USAJILI 

Na.  AINA YA MAOMBI KIWANGO
1.  Maombi ya kusoma rejist (perusal fee) 50,000
2 Maombi ya kupatiwa hati iliyothibitishwa na Msajili au kuidhinishwa hati inayoletwa na mdau 50,000
3 Maombi ya Kivuli cha cheti au hati nyingine iliyo katika hifadhi ya Baraza 50,000
4 Kuwasilisha marekebisho ya Katiba kwa Msajili 50,000
5 Kuwasilisha mabadiliko ya Viongozi wa Klabu, Chama au Shirikisho cha Michezo pale ambapo viongozi wamebadilika kwa sababu nyingine bila kubadili umiliki 10,000
6 Kuwasilisha mabadiliko ya umiliki wa klabu cha michezo pale ambapo klabu kimeuzwa kwa mtu au taasisi nyingine 2% ya mapato ghafi la mauziano
7 Maombi mengineyo 50,000