Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
Taratibu namna ya kusajili Chama/Mashirikisho/Taasisi za Michezo?
A. KUSAJILI KWA KUPITIA MFUMO WA SARS : SaRS ni mfumo wa kidigitali unaomwezesha mdau/mteja wa michezo kuweza kujisajili online, pamoja na kupata huduma zote zinazohusu usajili kwa kutumia mfumo. Mteja/mdau ataweza kujisajili kwa kutumia mfumo.
Taratibu za Kujisajili kwa Kupitia Mfumo wa SaRS:-
Mteja/Mdau wa Michezo anatakiwa afanya yafuatayo:-
i. Afungue akaunti katika mfumo wa SaRS ili aweze kuingia ndani ya mfumo
ii. Aingie ndani ya mfumo na kuweza kuchagua aina ya huduma anayotaka kuifanya. Huduma zilipo ndani ya mfumo huu wa SaRS ni:
a. Maombi ya Usajili (Application for registration)
b. Maombi ya kubadilisha katiba ( Correcting constitution)
c. Maombi ya kubadilisha kifungu ( Change ofn Articles)
d. Maombi ya kubadilisha Jina ( Change of Name)
e. Maombi ya kubadilisha anuani ( Change of Address)
iii. Kuwa na nakala laini ya viambatanisho muhimu vya Kusajili Vyama/Mashirikisho/ Taasisi za Michezo. Viambatanisho hivyo ni kama ifuatavyo:-
a. Nakala laini ya Muhtasari wa kikao cha wanachama kilichofikia uamuzi wa kuunda chama na kupitisha katiba.
b. Nakala laini ya Katiba.
c. Nakala laini ya Kanuni za fedha za chama.
d. Nakala laini ya Kanuni za uendeshaji wa shughuli za Chama
e. Orodha ya majina ya wanachama wake na namba za wanachama
f. TIN Namba
g. Cheti cha usajili wa Kampuni BRELA
h. Nakala laini ya sahihi za mwenyekiti pamoja na katibu wa chama .
iv. Nyaraka hizi laini zinatakiwa zipandishwe katika mfumo. Baada ya kukamilisha kupandisha taarifa, mdau/mteja ataweza kutengeneza control number ( namba ya malipo) ili aweze kulipia gharama za usajili au huduma atakayokuwa ameomba.
v. Baada ya kukamilisha malipo mteja atatoka nje ya mfumo na kusubiri taratibu za kusajiliwa zikamilike.
B. KUSAJILI KWA KUTUMIA UTARATIBU WA KAWAIDA
3.(I) Chama chochote kinachotaka kusajiliwa kitapeleka maombi yake kwa Msajili Msaidizi aliyeko katika Wilaya ambayo ni makao makuu ya chama hicho. Maombi haya yaambatanishwe na:
- Muhtasari wa kikao cha wanachama kilichofikia uamuzi wa kuunda chama,
- Katiba iliyopitishwa na kikao;
- Nakala tatu za Katiba ya chama;
- Nakala tatu za kanuni za fedha za chama;
- Nakala tatu za kanuni za uendeshaji shughuli za chama;
- Orodha ya majina ya uanachama wake na namba ya uanachama kwa msajili
(II) Baada ya kuwasilishwa maombi, Msajili Msaidizi aliyeoko katika Wilaya atawapatia viongozi wa chama Fomu Na. BMT 1 na Fomu Na. BMT 2 wazijaze na kisha kupelekwa kwa Msajili wa Vyama vya Michezo BMT
(III) Msajili akishayapokea maombi hayo, atayahakiki na endapo hataona upungufu wowote, atakisajili chama hicho kwa kufanya yafuatayo:
- Kuingiza jina la Chama katika daftari la Usajili wa Vyama vya Michezo; na
- Kutoa hati ya Usajili.
(IV) Endapo Msajili atabaini upungufu kwenye maombi yaliyowasilishwa kwake na Msajili Msaidizi, atawajulisha wahusika upungufu uliopo kwa kutumia Fomu Na. BMT 3 ili wakafanyie marekebisho.
(V) Endapo Msajili atakataa kukisajili chama, atatoa taarifa kwa chama husika kwa kutumia Fomu Na .4 BMT
(VI) Chama cha mchezo wowote hakitaruhusiwa kuendesha shughuli za Michezo bila kusajiliwa. Aidha, chama kilichosajiliwa hakiruhusiwi kuwa na ushirikiano wa kimichezo na chama ambacho hakijasajiliwa.
4(I) Kila katiba ya chama inatakiwa kuonyesha kwa uwazi mambo yafuatayo:
- Jina la Chama
- Anuani kamili, ikiwa na mate au kijiji, namba ya nyumba au ofisi, namba ya sanduku la Posta na Simu kama ipo na pia Mji, Wilaya na Mkoa.
- Idadi na aina ya michezo
- Muundo wa chama
- Wajibu na kazi za kamati mbalimbali.
- wajibu na kazi za viongozi na Wanachama
- Kalenda ya :
- Mikutano ya kamati ndogondogo;
- Mikutano ya kamati ya Utendaji;
- Mkutano Mkuu wa uchaguzi.
- Taratibu za kushughulikia migogoro na rufaa;
- Sifa za wagombea uongozi zimewekwa bayana kulingana na aina ya mchezo, utaalam, uzoefu, kiwango cha elimu na ngazi ya chama husika kwa mujibu wa sera ya maendeleo ya michezo.