AFRIKA KUSINI MABINGWA MASHINDANO YA BASEBALL 5 AFRIKA
service image
26 May, 2022

Timu ya Taifa ya Baseball ya Afrika Kusini imefanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya Baseball 5 kwa mataifa ya Afrika baada ya kuifunga timu ya Taifa ya Kenya katika mchezo wa Fainali uliochezwa uwanja wa ndani wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.

Kwa matokeo hayo Timu ya Afrika Kusini imefanikiwa kutinga katika mashindano ya Dunia baada ya kumaliza katika nafasi ya kwanza wakiungana na Kenya ambao wamemaliza katika nafasi ya pili.

Katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu, timu ya Taifa ya Tunisia imefanikiwa kuifunga Uganda ambayo imemaliza katika nafasi ya 4 na wenyeji Tanzania wakishika nafasi ya 5.
Mashindano hayo yamefanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe 23 hadi 26 Mei, 2022.