WANARIADHA WAKABIZIWA VIFAA VYA KUKIMBILIA

Shirikisho la Riadha Tanzania tarehe 08/10/2023 limekabidhi vifaa mbalimbali kwa timu m mbili za riadha zinazoenda kushiriki mashindano ya Kimataifa nchini Japan na Switzerland.
Team mojawapo iliyokabidhiwa vifaa ni team ya riadha ya JWTZ inayokwenda kushiriki mashindano ya Majeshi nchini Uswiss tarehe 29 na 30 Octoba 2023, makabidhiano hayo yalifanywa Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo wakili Jackson Ndaweka katika uwanja wa Shekh Amri Abeid Kaluta jijini Arusha.
Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi, Kamanda wa Kikosi cha 977 Col Khamis Kinguye amelishukuru shirikisho na kuwataka wachezaji kutendea haki heshima waliopewa.
Amewahakikishia wachezaji kwamba Jeshi na nchi kwa ujumla iko pamoja nao na wasimuangushe Amir Jeshi Mkuu na Rais wa Nchi Samia Suluhu Hassan.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni Viatu, tshirts, sox na Full track suit kwa wachezaji na viongozi, na nguo za kukimbilia(Running Kit) kwa wachezaji. Timu nyingine iliyokabidhiwa vifaa kama hivyo ni inayokwenda kushiriki Nagai Marathon nchini Japan
Makabidhiano hayo yalishuhudiwa na viongozi wa Chama cha Riadha Mkoa wa Arusha.