TIMU YA TAIFA YA VIJANA CHINI YA UMRI WA MIAKA 19 (U19) YAAGWA RASMI
service image
06 Jan, 2026

Tukio la kuaga Timu ya Taifa ya Vijana wa chini ya umri wa miaka 19 (U19) ya Kriketi lililofanyika leo Januari 6, 2026 katika ukumbi wa Four Points by Sheraton, jijini Dar es Salaam, kuelekea ushiriki wao katika Kombe la Dunia la Kriketi litakalofanyika nchini Namibia na Zimbabwe.

Hafla hiyo imewakutanisha viongozi wa michezo, wadau pamoja na wachezaji, ikiwa ni sehemu ya kuwapa hamasa na kuwatakia kila la heri vijana hao wanapoenda kuiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo makubwa ya kimataifa.