BMT YAKUTANA NA SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA (NIC)
service image
06 Jan, 2026

Baraza la Michezo la Taifa (BMT),leo Januari 6, 2026 limekutana na viongozi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) pamoja na wachezaji wa zamani, kwa lengo la kujadili namna wachezaji wanavyoweza kupata huduma ya bima ya mazishi.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika katika ofisi za BMT, Ofisa Michezo Mwandamizi wa Baraza hilo, Bw. Charles Maguzu, amesema mpango huo una lengo la kuwasaidia wachezaji kukabiliana na changamoto zinazojitokeza pindi wanapofiwa na ndugu au watoto wao.

Bw. Maguzu amesisitiza kuwa huduma ya bima ya mazishi itakuwa msaada mkubwa kwa wachezaji wa zamani na waliopo, kama sehemu ya jitihada za BMT kuhakikisha ustawi na heshima ya wanamichezo inalindwa hata baada ya kustaafu.