WAKUFUNZI WA MPIRA WA KIKAPU WANUFAIKA NA KOZI YA SHIRIKISHO LA MPIRA KIKAPU DUNIANI.
Wakufunzi wa mchezo wa Kikapu nchini wanufaika na mafunzo kutoka Shirikisho la Dunia Mpira wa kikapu 'International Basketball Federations' (FIBA) Level 1 kupitia kwa Shirikisho la Mpira wa kikapu Tanzania (TBF) yaliyoendeshwa na Mkufunzi Craig Daniel kutoka Afrika ya Kusini kuanza tarehe 28 Mei hadi tarehe 2 Juni, 2024 katika Kituo cha Michezo cha vijana cha Jakaya Mrisho Kikwete (JKM) jijini Dar es Salaam.
Mafunzo hayo yalijumuisha makocha 15 kutoka Taasisi mbalimbali na maeneo mbalimbali ya nchi ikiwemo Kigoma, Mbeya, Tanga, Tabora, Unguja na wenyeji Dar es salaam, ambapo washiriki kutoka Pemba, Pwani, Iringa na Arusha hakuweza kushiriki kutokana sababu mbalimbali.
Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea wakufunzi wa ndani walioshiriki katika kuwajengea uwezo zaidi wa kufundisha mchezo huo
Aidha Shirikisho la Mpira wa kikapu nchini (TBF ) linatarajia kuendelea kuwapiga msasa makocha ili kupata elimu bora kwa manufaa ya Mpira wa kikapu nchini.