BMT NA BASATA YAFANYA KIKAO CHA PAMOJA.
service image
15 Jan, 2026

Maafisa kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) leo Januari 15,2026 wamekutana na kufanya kikao cha pamoja chenye lengo la kujengeana uwezo na kuimarisha ushirikiano katika masuala mbalimbali yanayohusiana na sekta ya michezo na sanaa nchini.

Kikao hicho kimefanyika katika ofisi za Baraza la Michezo la Taifa (BMT), ambapo pande zote mbili zimejadili maeneo ya ushirikiano yatakayosaidia kukuza vipaji, kuboresha mifumo ya kazi, pamoja na kuendeleza fursa za kiuchumi zitokanazo na michezo na sanaa.

Katika kikao hicho wamekubaliana kuimarisha mashirikiano ya kitaasisi, kubadilishana uzoefu na utaalamu, pamoja na kuweka mikakati ya pamoja itakayosaidia kuleta tija kwa maendeleo ya sekta hizo mbili muhimu kwa taifa ambapo
hatua hiyo inaonesha dhamira ya BASATA na BMT katika kuhakikisha michezo na sanaa vinaendelea kukua, kuimarika na kuchangia maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini Tanzania.