BMT YA PAMBA MOTO NA MICHEZO KWA JAMII

Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo Wilaya ya Muheza Ndugu Nelson Kasiti ( shati jeupe) akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa wa Baraza la Michezo la Taifa pamoja na Wakufunzi wa michezo mbalimbali walipowasili Januari 13, 2025 ofisini kwake kujitambulisha na kupata ridhaa ya kufundisha michezo ya Mpira wa miguu, Netiboli, Riadha, Kikapu na Wavu chini ya Mpango wa Mafunzo ya Michezo kwa Jamii ( Community Sports).
Mafunzo hayo yanaratibiwa na BMT kwa kushirikiana na Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania ambayo yatafanyika kuanzia tarehe 13 Januari, 2025 hadi tarehe 17 Januari, 2025
Aidha Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo Wilaya ya Muheza ameipongeza BMT kwa kuchagua Wilaya ya Muheza kuwa moja ya Wilaya nchini zilizopewa fursa ya kupata mafunzo hayo.