BMT yakutana na waandaaji wa Ramadhan Cup 2026
service image
17 Jan, 2026

Wataalam wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) wakiongozwa na Kaimu Katibu Mtendaji Bw. Benson Chacha, Januari 16, 2026 wamekutana na kufanya kikao na waandaaji wa mashindano ya Ramadhan Cup 2026, wakiongozwa na Ally KibaRais wa Crown Media katika ofisi Crown zilizopo Mikocheni, jijini Dar es Salaam.

Kikao hicho kililenga kujadili na kuandaa mpango wa mashindano ya Ramadhan Cup, hususan katika maeneo ya uendeshaji, usimamizi pamoja na ugharamiaji wa mashindano hayo. Hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo lililotolewa na Mhe. Paul Makonda, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo alipokutana na waandaaji hao hivi karibuni, jijini Dodoma.

Mashindano ya Ramadhan Cup, ambayo yanalenga kukuza umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi pamoja na kutoa burudani katika kipindi cha Mfungo wa Ramadhan, yanatarajiwa kufanyika katika mikoa mitano nchini, itakayobainishwa rasmi hivi karibuni.