KONGAMANO LA WADAU WA MICHEZO KUELEKEA CHAN NA AFCON

15 Jan, 2025
Kamisheni Mtendaji wa kituo cha Ubia baina ya Sekta ya umma na sekta binafsi (PPPC) David Kafulila amewaita wawekezaji kuchangamkia fursa ya kuwekeza kwenye maeneo mbalimbali ya huduma za kijamii kuelekea mashindano ya chan na Afcon.
Rai hiyo imetolewa leo Januari 15 2025 katika hafla ya kongamano la wadau wa Michezo kuelekea CHAN 2024 na AFCON 2027.
Amesema kuwa wahakikishe wanaleta maandiko ya ubia ili kituo cha cha ubia baina ya sekta ya umma na binafsi kiweze kuyafanyia kazi.
“Wawekezaji hii ni fursa ya kutoa huduma hususani katika mashindano hayo,” amesema.