MSIMU WA NNE WA TAMASHA LA MICHEZO LA WANAWAKE (TANZANITE)

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limeandaa Msimu wa nne (4) wa Tamasha la Michezo la wanawake (Tanzanite women's Sports Festival 2025) ambalo kwa mwaka huu linafanyika Mkoani Arusha.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo Machi 06, 2025 Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo Bi. Neema Msitha alisema kuwa, tamasha la mwaka huu litahusisha mambo kadhaa ikiwemo fainali ya shindano la 'Tanzanite Samia Women's Super Cup' litakalohusisha timu ya Yanga princes dhidi ya JKT Queen, itakayofanyika Machi 06, 2025 pamoja na kutembalea kituo cha kuibua na kukuza vipaji vya wachezaji wanawake cha Orkeeswa Wilayani Mondoli.
Aliongeza kuwa, Machi 07, 2025 Tanzanite itapamba na kongamano wa wadau wa Michezo wanawake litakalohusisha elimu sambamba na hadithi za mafanikio ya wanawake waliofanya vizuri kupitia sekta ya michezo,
Kauli mbiu ya msimu wa nne wa Tamasha hilo ni 'Jasiri Uwanjani, Jasiri Maishani