HAPPY INTERNATIONAL WORKER'S DAY

01 May, 2024
Wafanyakazi wa BMT leo Mei Mosi, 2024 wameungana na wafanyakazi wa taasisi zingine za serikali pamoja na sekta binafsi za Mkoa wa Dar es salaa katika maandamano ya maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani yaliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru.
Maadhimisho ya mwaka huu yamepambwa na ujumbe usemao "Nyongeza ya Mishahara ni Msingi wa Mafao Bora na Kinga dhidi ya hali ngumi ya Maisha'.
Aidha, wafanyakazi wa Baraza nao wameongeza kwa kuwapa watanzania ujumbe usemao ' Shiriki michezo kuimarisha afya ili kuipambania Tanzania katika uchumi Imara'.
Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo Mkoa huo ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila.