MABONDIA WAJINOA KUPITIA MAPAMBANO YA KIMATAIFA KUJIANDAA NA MASHINDANO YA JUMUIYA YA MADOLA
service image
30 May, 2022

Mabondia wa timu ya Tanzania wanaojinoa kuelekea katika michezo ya Jumuiya ya Madola leo Mei 29, 2022 wameonesha viwango vyao kimataifa baada ya kuwacharanga mabondia wa Burundi kwa pointi katika mapambano ya kimataifa ya majaribio yanayoendelea katika Uwanja wa Benjamin Jijini Dar es salaa.
Shaibu Baruti mwenye uzito wa (Light Weight 60 Kg amempiga kwa pointi 3-0 mpinzani wake Djafari Nshmirimana huku Alex Isendi uzito wa (Light Welter 63.5 akiibuka na ushindi wa pointi 3-0 dhidi ya Mahataneeric wote kutoka Burundi.

Mwingine ni Bondia Elius Damson aliyeibuka na Ushindi pointi 2-0 dhidi ya mpinzani wake Rally Zrkoze naye kutoka Burundi waliopigana katika uzito wa (Welter Weight 67 Kg).
Pambano la awali liliwakutanisha mabondia wa kike Magrethy Itembo kutoka Zambia aloyeibuka na pointi 3-0 dhidi ya Teddy Nakumul kutoka Uganda, huku Mwendo Mwale kutoka Zambia akitwaa pointi 3-0 dhidi ya bondia Kassim Ally kutoka magereza.

Wengine ni bondia Andrew Chilata kutoka Zambia aliyeibuka na pointi 3-0 dhidi ya Shabani Mganda kutoka Jeshi la Kujenga Taifa. Bondia Tukumuhebwa kutoka Uganda aliyeibuka na pointi 3-0 dhidi ya Joseph John kutoka Magereza, Mwande Shapt kutoka Zambia aliyemshinda kwa pointi 3-0 Shaban Hamadi wa Jeshi la Magereza.
Kibira Owen kutoka Uganda aliyempiga kwa (KO) Sabura Fransis wa JKT uzito wa 67 kg huku uzito wa (71 Kg Light middle) Ziuba Stephan kutoka Zambia akimpiga kwa pointi 2-0 Kassim Mbudwike (Taifa), Yusuph Ally Magereza hakufika kwa bondia Senyange Zebra kutoka Uganda.

Wakati Joseph Philip bondia kutoka timu ya Jeshi la Magereza akifunga dimba la pambano la Mei 29 kwa kumtwanga kwa pointi 3-0 bondia Nduwarugila Nestory kutoka Burundi.
Mapambano hayo yameshirikisha mabondia wakiume 5 na wakike mmoja kutoka Uganda, Mabondia wakiume 6 kutoka Tanzania, mabondia wakiume 10 na wakike 6 kutoka JKT, mabondia wakiume watano na wakike (4)kutoka Zambia, huku Burundi wakiwakilishwa na mabondia wakiume (6) na wakike (2) na wakati Jeshi la Magereza wakiwakilishwa na mabondia wakiume nane (8).