MAFUNZO KARATE YAINGIA SIKU YA PILI
service image
05 Oct, 2022

Mafunzo na Semina ya Siku saba kwa wanakarate maarufu kwa jina la (GASHUKU) leo Oktoba 05 yameingia siku ya pili katika ukumbi wa Starlight Arena Jijini Dar es salaam

Mafunzo hayo yanaendeshwa na Wataalamu wa Mchezo wa Karate kutoka Japani, Shihan Naka pamoja na Shihan Okuma .

Zaidi ya mataifa 35 yanashiriki katika mafunzo na semina hiyo likiwemo taifa la Ujerumani, China na mataifa ya Barani ya Bara la Afrika.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Said Yakub anatarajiwa kufunga mafunzo hayo tarehe 09 Oktoba ambapo yatahitimishwa na Mashindano ya mchezo huo kwa nchi shiriki.