MAPAMBANO YA MAJARIBIO KIMATAIFA YAKAMILIKA
service image
31 May, 2022

Fainali ya mashindano ya majaribio ya kimataifa ya Ngumi za Ridhaa yamekamilika tarehe 31 Mei, 2022 kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa Jijini Dar Es Salaam,katika fainali hiyo jumla ya mapambano 15 yalipigwa yalishirikisha wanawake na wanaume.

Katika uzito wa 63.5kg bondia wa timu ya Taifa Alex Isendi alipoteza kwa RSCI dhidi ya Joseph John kutoka Magereza, huku Emmanuel Katema wa Zambia akipoteza kwa DSQ dhidi ya Tukamuhebwa kutoka Uganda.
Naye bondia Shaibu Baruti akikubali kipigo cha pointi 3-0 dhidi ya Andrew Chilata wa Zambia katika uzito 60kg.

Katika uzito wa 71kg Ziuba Stephan wa Zambia alishinda kwa pointi 2-1 dhidi ya Kasim Mmbundike wa timu ya taifa Tanzania.
Huku katika uzito wa 75kg Kevin Kipinge wa timu ya Taifa naye akipoteza pambano kwa TKO dhidi ya Nkobeza Yusuph wa Uganda, huku katika uzito wa 67kg Mwande Shaft wa Zambia aliibuka na ushindi wa pointi 2-1 dhidi ya Kibira Owen wa Uganda na uzito wa 52kg Chinyemba Patrick wa zambia amemtwanga kwa pointi mpinzani wake Nimubona Mussa kutoka Burundi.
Uzito wa 48kg Abdallah Maganga wa JKT ameshinda kwa pointi 3-0 dhidi ya Fadhili Hassan wa Magereza.

Kwa upande wa wanawake uzito wa 48kg Elizabeth Phil wa Zambia ameshinda kwa pointi 3-0 dhidi ya Rahma Joseph wa JKT, huku Teddy Nakumuli wa Uganda ameibuka na ushindi wa pointi 3-0 dhidi ya Magret Tembo wa Zambia katika uzito wa 52kg.

Uzito wa 54kg Havyarimana Oreneneka wa Burundi amekubali kichapo cha RSCH dhidi ya Hilda Ng'andue wa Zambia, wakati uzito wa 54kg Beatrice Ambros wa JKT amepoteza kwa W/O dhidi ya Lilian Paul wa Zambia na Peatus Kandi wa Zambia amepata ushindi wa RSCH dhidi ya Grace Amos wa JKT katika uzito wa 63kg.