MDAHALO KATIKA WIKI YA VIJANA KITAIFA KAGERA
service image
10 Oct, 2022

Vijana wametakiwa kuimarisha ushirikiano, mshikamo na mawasiliano ili kufikia malengo ya dira na maono yao katika kujenga uchumi imara.

Hayo yameelezwa leo Oktoba 10, 2022 katika mdahalo uliohusisha wawezeshaji wa mada mbalimbali ili kuwajengea vijana uwezo wa kujenga uchumi imara kwa maendeleo endelevu, mdahalo ulifanyika Mkoani Kagera katika kuadhimisha wiki ya vijana kitaifa.

Katika mada ya afya vijana wametakiwa kushiriki katika michezo ili kujenga afya zao na kuweza kutekeleza majukumu yao kwa umakini na ufanisi kwa maendeleo endelevu.



"Michezo ni Afya, Ajira na hujenga mahusiano mazuri ambapo mnaweza kujadiliana mengi kufikia uchumi imara na endelevu,"alisema Afisa Uhusino wa BMT wakati akichangia mada ya afya kwa vijana.

Kauli mbiu katika maadhimisho hayo ni"Kila mmoja anahusika Kujenga Uchumi Imara na Ustawi wa Maendeleo Endelevu.