MHE. GEKUL AWATAKA AT KUALIKA NCHI NYINGI ZAIDI MASHINDANO MENGINE YA RIADHA AFRIKA MASHARIKI

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul amewataka Viongozi wa Shirikisho la Riadha Tanzania (AT) kualika nchi nyingi zaidi pamoja na kuwaandaa wachezaji wengi kushiriki mashindano mengine yatakayofanyika nchini.
Rai hiyo ameitoa wakati akifungua mashindano ya riadha ya vijana wa umri chini ya miaka 18 na chini ya miaka 20 kutoka katika nchi za Afrika Mashariki na Kati yatakayofanyika kwa siku mbili (2) kuanzia tarehe 27- 28 Mei, 2022 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijjini Dar es salaam.
"Karibuni sana majirani zetu katika mashindano mengine yajayo, nchi yetu ni salama na hali ya hewa ni nzuri, AT mashindano mengine alikeni nchi nyingi zaidi," alisema, Mhe Gekul na kuongeza kuwa!
"Naamini kila mmoja amekuja kushiriki akiamini atashinda pia, nchi zenu zimewaamini na kutegemea kushinda, naamini kila mmoja atakuwa mshindi, mimi nawatakia maahindano mema,"alisema.
Mashindano hayo ya riadha kwa Vijana wa umri huo ya nchi za Afrika Mashariki na Kati yamehusisha nchi saba ikiwemo mwenyeji Tanzania, Sudan Kusini, Somalia, Kenya, Ethiopia, Eritrea, Zanzibar