MHE. MAKONDA AWASILI NCHINI MOROCCO
service image
18 Jan, 2026

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amewasili nchini Morocco kwa ziara maalum ya kikazi akiwa na jukumu la kuwasilisha ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan, kwenda kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Dk. Patrice Motsepe.

Ziara hiyo inalenga kuimarisha ushirikiano wa kimkakati katika sekta ya michezo, hususan maendeleo ya mpira wa miguu barani Afrika na nafasi ya Tanzania katika michuano na programu mbalimbali zinazosimamiwa na CAF.