MHE. RAIS AKABIDHIWA JEZI YA TIMU YA TAIFA.
service image
10 Jan, 2026

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amepokea zawadi ya jezi ya Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanaume ‘Taifa Stars’ iliyosainiwa na wachezaji, kutoka kwa nahodha msaidizi wa timu hiyo, Bakari Nondo Mamnyeto, katika hafla maalum ya kuwapongeza wachezaji na viongozi wa Taifa Stars, iliyofanyika Ikulu, Jijini Dar es Salaam, tarehe 10 Januari 2026.

Tukio hilo lilikuwa sehemu ya kutambua na kuthamini mchango wa timu hiyo katika kuiwakilisha vyema Tanzania kimataifa na kuandika historia mpya katika mashindano ya soka barani Afrika.