MSITHA AIPA SIKU 5 RT.

Msitha aipa siku 5 RT kuwasilisha taarifa ya kufanyika kwa mkutano Mkuu wa mwaka, kufanyika mashindano ya Riadha Taifa, Hali ya Fedha pamoja na Taarifa ya Mkakati wa muda mrefu wa RT
Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Neema Yotham Msitha, ameipa siku tano (5) kamati Tendaji ya Shirikisho la Mchezo wa Riadha Tanzania (RT), kuwasilisha taarifa ya mbalimbali za kiutendaji ikiwemo ya kufanyika kwa mkutano Mkuu wa mwaka, kufanyika mashindano ya Riadha Taifa, Taarifa ya Hali ya Fedha pamoja na Taarifa ya Mkakati wa muda mrefu wa RT.
Msitha ametoa maagizo hayo leo tarehe 30 Septemba, 2022 alipokutana na viongozi wa kamati Tendaji ya RT katika moja ya kumbi za uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, ambapo amesisitiza kuwa umoja na mshikamano wa viongozi na wadau ndio chachu pekee itakayoendelea kuleta mafanikio zaidi katika mchezo wa Riadha.
“nawapa siku 5 mpaka Jumanne ya tarehe 4 Oktoba, 2022 kuwasilisha taarifa ya mbalimbali za kiutendaji ikiwemo ya kufanyika kwa mkutano Mkuu wa mwaka, kufanyika mashindano ya Riadha Taifa, Taarifa ya Hali ya Fedha pamoja na Taarifa ya mkakati wa muda mrefu wa RT, ”alisema Msitha.
Aidha Msitha ameutaka uongozi wa RT kuhamasisha kuundwa kwa Chama cha Makocha na Waamuzi, kuboresha kanuni za mbio ndefu (Marathon) na kuwasilisha BMT kanuni hizo pamoja na kuzingatia mgawanyo wa majukumu miongoni mwa watendaji kwa mujibu wa Katiba ya RT.
Kwa upande mwingine Msitha ameupongeza uongozi wa RT kwa uboreshaji wa Uhusiano baina ya Tanzania Bara na Visiwani katika mchezo wa Riadha.