MSITHA ATOA RAI WAWEKEZAJI KUWEKEZA KATIKA MICHEZO
service image
07 Oct, 2022

Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Neema Msitha atoa rai kwa wawekezaji kuona fursa ya kuwekeza katika michezo.

Rai hiyo ameitoa leo Oktoba 06, 2022 wakati wa mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na viongozi wa Chama cha mchezo wa kuogelea (TSA) kuuhabarisha umma juu ya Mashindano ya kanda ya tatu (3) yanayotarajiwa kufanyika Novemba 15 mpaka 20 kwenye bwawa la kuogelea la klabu ya Gymkhana huku Tanzania ikiwa mwenyeji kwa mara ya pili katika historia.



“Naipongeza TSA kwa kupewa heshima kubwa ya kuandaa mashindano haya. Ni faraja kwa nchi kwani mbali ya kuitangaza nchi, pia inatoa fursa kwa wachezaji wetu kupima viwango vyao kimataifa na vile vile kuutangaza utalii wa nchi,” alisema Msitha.

Jumla ya nchi 25 zinatarajia kushiriki katika mashindano hayo ikiwemo, Burundi, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Somalia, Sudan, Sudani Kusini, Uganda na Tanzania kwa nchi za kanda ya tatu Afrika.

Nchi za kanda ya Nne Afrika ambazo zinatarajia kushiriki katika mashindano hayo ni Angola, Botswana, Comoros, Lesotho, Madagasca, Malawi na Afrika Kusini.