MSITHA AFANYA MAZUMGUMZO YA NAMNA YA KUANZISHWA KWA MCHEZO MPYA NCHINI
service image
03 Oct, 2023

Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Neema Msitha amefanya mazungumzo ya namna ya kuanzishwa kwa mchezo mpya nchini ujulikanao kwa jina la "Sports Gymnastics".

Bi Msitha amekutana na wajumbe hao Ofisini kwake leo Oktoba 03, 2023 na kufanya mazungumzo, ambapo alipata maelezo ya kina kutoka kwa wachezaji na mtaalam huyo aliyetembelea Tanzania kama sehemu ya ziara yake ya kuenezi mchezo huo.

Mtaalam huyo mwenye jukumu la kuuendeleza mchezo huo katika Afrika alitembelea BMT akiongozana na Bw. Frank Mhina na Laurence Cheyo ambao ni wachezaji wenyeji wanaobeba dhamana ya kuueneza mchezo huo hapa nchini kwa lengo la kubadilishana mawazo na Viongozi hao juu ya namna bora ya kuendeleza mchezo huo ambao kwa miaka mingi umekuwa ukifananishwa na sanaa za sarakasi (Acrobatics).

Aidha, Msitha amewataka wadau hao wa Gymnastic kuhakikisha wanawasilisha kanuni za mchezo na kufuata taratibu zote za kuusajili, kutambua waendeshaji wa mchezo pamoja na kuhamasisha washiriki wote wa hapa nchini wajisajili kabla ya kuanza shughuli za kuufundisha na kuusambaza katika maeneo mbalimbali ya nchi ili wapate wanachama wakutosha kuunda vilabu na hatimaye chama cha Taifa.