MTWARA YATAMBA KWA UNGUJA NETIBOLI UMITASHUMTA 2023
Timu ya Netiboli ya Mkoa wa Mtwara imeibuka na ushindi mnono baada ya kuifunga Kanda ya Unguja jumla ya magoli 24 – 11 katika mchezo uliochezwa Asubuhi ya tarehe 7 Juni 2023 kwenye viwanja vya Shule ya Wasichana Tabora.
Mchezo mwingine ulizikutanisha timu za Mikoa ya Shinyanga na Iringa, ambao ulimalizika kwa Iringa kukubali kipigo cha magoli 34 – 05 huku Mkoa wa songwe ukiiadhibu Dar es salaam kwa magoli 37 – 24.
Wakati huohuo Timu ya mkoa wa Singida imeibuka na ushindi wa magoli 32 – 19 dhidi ya Mkoa wa Njombe, na Manyara ikakubali unyonge kwa Mkoa wa Kavi kwa kufungwa magoli 24 - 14.
Ushindi mkubwa zaidi katika michezo ya Netiboli iliyochezwa asubuhi ulikuwa ule wa Mkoa wa Mwanza ambao Uliishinda Kilimanjaro magoli 52 -07, na wenyeji Tabora kuendeleza ubabe kwa kuifunga Mbeya 16 - 10.
Mashindano ya UMITASHUMTA 2023 yaliyoanza Juni 03, 2023 imeingia siku 05 Mkoani Tabora inakofanyika kitaifa, ikihusisha michezo ya mpira wa Netibali, Wavu (wasichana na Wavulana), Mpira wa miguu kawaida (Wasichana na wavulana), Mpira wa miguu wavulana (Maalum) na Mpira wa mikono – Handball (kawaida).
Vilevile inahusisha Mchezo wa kuruka chini, Riadha (kwaida na maalum) Mpira wa Goli (Goal Ball) mahususi kwa wenye uono hafifu, Mpira wa kikapu (Wasichana na Wavulana) na Sanaa za michezo zinazojumuisha uimbaji na uchezaji wa ngoma za asili.