*MWAKA MMOJA WA MAMA SAMIA WATENDAJI BMT WAENDELEA KUAMINIWA KATIKA KUINUA SEKTA YA MICHEZO NCHINI*

Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mhe. Samia Sukuhu Hassan ikiwa imetimiza mwaka mmoja wa Uongozi wake, umeendelea kuwaamini watendaji wa Baraza la Michezo la Taifa kwa kuwathibitisha watendaji wakuu wa Baraza hilo.
Watendaji waliothibishwa kutumikia nafasi zao ambazo walikuwa wakizikaimu Kwa muda mrefu ni pamoja na Neema Msitha ambaye amethibishwa kuwa Mtendaji wa Baraza hilo na Consolata Mushi kuwa Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) huku akimteua Riziki Majala kuwa Msajili wa Vyama vya Michezo.
Akiongea Katika Kongamano la wadau wa Michezo la Mafanikio ya Sekta ya Michezo ndani ya mwaka mmoja wa serikali ya awamu ya sita, Leo tarehe 29, jijini Dar es salaam. Waziri mwenye dhamana ya Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Kutokana na ufanisi wa utendaji wa Baraza hilo, Kwa mamlaka aliyopewa ameamua kuwathibisha Viongozi hao ili jitihada za Baraza ziwe endelevu.
Mhe.Mchengerwa amebainisha kuwa ameamua kumrudisha aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa. BMT, Bw. Leodiger Tenga aendelee na wadhifa huo.
Aidha, wajumbe wake ni: Prof.Mtambo Mkumbwa- Mkurugenzi wa Kituo Cha kulea Vipaji vya Michezo Morogoro, Bw. Ally Mayai- Mdau wa Michezo, Yusuph Singo-Mkurugenzi wa Michezo , Ameir Makame-Kamishna wa BMZna Tuma Dandi - Rais wa Paralimpiki. Ameongeza kuwa wajumbe wengine watatangzwa pindi mchakato ukikamilika.