SEMINA YA MÇHEZO WA KARATE UJULIKANAO KWA JINA LA GASHUKU KWA LUGHA YA KIJAPANI IMEANZA LEO OKTOBA 04, 2022

04 Oct, 2022
Semina ya mçhezo wa Karate ujulikanao kwa jina la Gashuku kwa lugha ya kijapani imeanza leo Oktoba 04, 2022 katika ukumbi wa Star light Arena, jijini Dar es salaam.
Semina hiyo inaendeshwa na wakufunzi wawili kutoka nchini Japani, ambao ni Sensei Shihani Okuma na Sensei Shihani Naka.
Semina hiyo ya mafunzo ya Karate inashirikisha wàchezaji kutoka mataifa zaidi ya 35 duniani na
inatarajiwa kuhitimishwa tarehe 9 Oktoba 2022.
Aidha, Katika kuhitimisha mafunzo hayo, washiriki hao watakuwa na mashindano siku hiyo.