SERIKALI YA AWAMU YA SITA NA MAENDELEO YA MICHEZO NCHINI
service image
19 Oct, 2023

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro amesema Serikali ya awamu ya sita imejipambanua katika kuendeleza michezo kwa manufaa ya nchi, klabu na wachezaji.

Alisema wanatumia mchezo huo kujiweka kwenye ramani nzuri kama nchi, kuandika  historia kwa sababu ni kwa mara ya kwanza mashindano hayo kuanzia Tanzania.

"Sasa hivi wageni wako wengi, tunapokea marais 54 wa mashirikisho barani Afrika na Ujio huu utanufaisha kila mtu hapa nchini na kuinua uchumi, mechi sio ndogo, ukiangalia Simba ni timu ya saba unakutana na timu iliyokuwa ya kwanza katika msimamo wa Afrika. Hii mechi kwa wachezaji wa Simba ni kipimo tosha wa kuona ubora wao.

Lakini pia unaona jinsi gani mashindano haya yalivyombeba kila mtu kwa sababu msanii wa Tanzania Ally Kiba atakuwa sehemu ya kuwapa burudani ya muziki kwa wageni watakashuhudia mchezo huo," alisema Waziri Ndumbaro. 

Aliongeza kuwa  Tanzania imepata heshima nyingine kwa mchezo wa TP Mazembe dhidi ya Esperance mechi ambayo itachezwa hapa nchini katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Oktoba 22, 2023.