SHIMIWI YAENDELEA KUSHIKA KASI JIJINI TANGA

Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali na Mikoa (SHIMIWI), yameendelea kushika kasi kwa michezo mbalimbali kuchezwa katika viwanja tofauti, ambapo timu ya mchezo wa Netiboli ya wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imeendelea kutamba baada ya kuifunga timu ya Mkoa wa Mbeya (RAS MBEYA) kwa magoli 19-7 mchezo uliochezwa katika uwanja wa Bandari jijini Tanga.
Kwa upande wa mchezo wa kamba wanaume, timu ya wizara yenye dhamana ya michezo imepoteza kwa mara ya kwanza dhidi ya timu ya Maliasili baada ya kukubali kuvutwa mara mbili katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Usagara.
kwa upande wa timu nyingine matokeo ya kamba wanaume ni kama ifuatavyo;
Bunge 0 vs Nec 2
Katiba 0 vs Uchukuzi 2
Mahakama 2 vs Ikulu 0
Elimu 2 vs Ujenzi 0
kwa upande wa timu nyingine matokeo ya kamba wanawake ni kama ifuatavyo;
Bunge 0 vs Ujenzi 2
Viwanda 2 vs Ras Singida 0
MSD 0 vs Tamisemi 2