TANZANIA mabingwa wa mashindano ya mpira wa miguu ukanda wa Afrika Mashariki
service image
02 Oct, 2025

Timu ya Umoja wa Maveterani wa soka Tanzania (UMUSOTA) imetwaa ubingwa wa mashindano ya mpira wa miguu kwa ukanda wa Afrika Mashariki ‘The East Africa Legends Football Tournament’ baada ya kuifunga Timu ya Kenya kwa goli 1 – 0, mfungaji pekee goli hilo ni Mohamed Hussein.

Mashindano hayo yameshirikisha Nchi sita ambazo ni Burundi, Tanzania, Uganda, Rwanda, Sudani Kusini na wenyeji Kenya ikiwa ni kuadhimisha kilele cha siku ya Wazee Duniani yaliyofanyika nchini Kenya tarehe 1 Oktoba, 2025.