TANZANIA YAFUZU 16 BORA KOMBE LA DUNIA, MCHENGERWA AZINDUA KINOGESHO CHA #LETENIMZUNGU
service image
04 Oct, 2022

Timu ya Taifa ya Tanzania, Tembo Warriors, imefuzu kuingia 16 Bora ya Fainali za Dunia za Soka la Walemavu baada ya kumaliza ikiwa na pointi nne katika kundi lake ikiwa ya tatu nyuma ya Poland na Uzbekistan.

Tembo Warriors imekata tiketi hiyo baada ya kuwa moja ya timu nne zilizoshika nafasi ya tatu zikiwa na uwiano mzuri (best looser) baada ya kuifunga Uzbekistan, kutoka sare na Hispania na kufungwa na Poland.



Sasa Tembo Warriors watasubiri ratiba kujua timu gani ya kucheza nayo Jumatano Oktoba 5, 2022, kusaka tiketi ya robo fainali.

Akizungumza jioni hii katika chakula cha jioni kilichoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania hapa Istanbul, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohammed Mchengerwa amewataka vijana hao kuendelea kulishamirisha Taifa huku akizindua kampeni ya kuzifunga kila timu zinazokuja mbele yao iitwayo #LeteniMzungu.