TIMU YA KAMBA WANAUME YA WIZARA YA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO USO KWA USO NA VIWANDA HATUA YA 16 BORA

05 Oct, 2023
Timu ya kamba wanaume ya wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imepangwa kucheza na timu ya wizara ya viwanda katika mchezo wa kuvuta kamba hatua ya 16 bora katika mashindano ya SHIMIWI yanayoendelea Mkoani Iringa, baada ya kuongoza katika kundi D lililokuwa na timu za Idara ya Mashtaka, Maji na wakili Mkuu.
Mchezo huo wa hatua ya 16 bora utachezwa tarehe 6 Oktoba, 2023 katika uwanja wa Chuo cha Mkwawa.