SERIKALI YAMPOKEA SHAURI KWA SHANGWE

26 Sep, 2023
Serikali ikiwakilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongela pamoja na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) leo Septemba 26, 2023 wamewaongoza wananchi wa Mkoa huo katika mapokezi ya mwanariadha Magdalena Shauri mshindi wa tatu katika mashindano ya mbio ndefu (Marathon) yaliyomalizika Septemba 24, 2023 Berlin nchini Ujerumani.
Mapokezi hayo yalifanyika katika Uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA) Mkuu wa Mkoa pia, aliambatana na Katibu Tawala wa Mkoa Missaile Mussa, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania Jackson ndaweka, Kanali kinguye aliyemwakilisha CDF na viongozi mbalimbali wa chama na serikali wakionesha furaha zao katika mafanikio ya sekta ya michezo nchini.