TIMU YA KAMBA WANAUME WIZARA YA UTAMADUNI YAWAVUTA ARDHI

07 Oct, 2022
Timu ya kuvuta Kamba wanaume ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imefanikiwa kutinga katika hatua ya 16 bora baada ya kuibuka na ushindi kwa kuwavuta timu ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa mivuto 2-0.
Mchezo huo umechezwa katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Usagara mapema Oktoba 7, 2022 ikiwa ni muendelezo wa mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali na Mikoa (SHIMIWI) yanayoendelea jijini Tanga.