TLGU WAIBUKA KIDEDEA MASHINDANO YA AFRIKA MASHARIKI NA KATI
service image
04 Nov, 2023

Timu ya Tanzania ya Gofu Wanawake imeendelea kuonesha uwezo wao baada ya kutetea ubingwa wao katika Michuano ya Afrika Mashariki na Kati yaliyofanyika kuanzia tarehe 01 hadi 03 Novemba, 2023 Kigali nchini Rwanda.

Wachezaji walioipeperusha bendera ya Tanzania kwa ushindi katika michuano hiyo ni Neema Olomi, Vicky Elias, Hawa Wanyeche na Madina Iddi.