TSA WATAKIWA KUWASILISHA TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI ILIYOKAGULIWA

23 Oct, 2023
Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Neema Msitha, ameuagiza uongozi wa Chama cha kuogelea Tanzania (TSA) kuhakikisha wanakabidhi BMT taarifa ya mapato na matumizi iliyokaguliwa kwa kipindi cha miaka minne (4) iliyopita.
Msitha ametoa agizo hilo leo tarehe 23 Oktoba, 2023 alipokutana na uongozi huo ofisini kwake uwanja wa Benjamin mkapa Dar es Salaam ili kujadili mwenendo wa Chama hicho, ambapo amesema ni muhimu kila Chama au Shirikisho la mchezo kuwa na taarifa ya mapato na matumizi iliyokaguliwa kabla ya kufanya mkutano Mkuu wa Chama.