TWIGA STARS YAENDELEA KUPIGA MWINGI CECAFA

04 Jun, 2022
Timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars) imeendelea kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kwa kutokupoteza mchezo wowote katika mashindano ya ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) baada ya kulazimishwa sare ya kufungana magoli 2-2 dhidi ya Timu ya Taifa ya Ethiopia mchezo uliochezwa leo tarehe 4, Juni 2022 katika uwanja wa Njeru nchini Uganda.
Magoli ya Tanzania yamefungwa na mchezaji Opa Clement pamoja na Enekia Lunyamila.
Twiga Stars sasa itakutana na ndugu zao Zanzibar katika mchezo wa 3 utakaochezwa tarehe 6 Juni, 2022, mchezo ambao utaiwezesha timu hiyo kutinga katika hatua ya nusu fainali ya mashandano hayo.