TWIGA STARS YAPANGWA KUNDI B, WAFCON 2026
15 Jan, 2026
Timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania, Twiga Stars, imepangwa katika Kundi B la Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) 2026, sambamba na timu za Afrika Kusini, Ivory Coast (Côte d’Ivoire) na Burkina Faso.
Droo hiyo imefanyika leo jijini Rabat, Morocco, ikiwa ni ishara rasmi ya kuanza safari ya mashindano yanayotarajiwa kufanyika kuanzia Machi 17 hadi Aprili 3, 2026, nchini Morocco

