USAILI WA CHAMA CHA MCHEZO WA JUDO TANZANIA
16 Jan, 2026
Usaili wa kuwapata viongozi wa Chama cha Mchezo wa Judo Tanzania (JATA) umefanyika leo, Januari 16, 2026, katika ukumbi wa Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.
Usaili huo umefanyika ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi wa viongozi wa chama hicho, unaotarajiwa kufanyika Januari 17, 2026, katika ukumbi huohuo wa Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Mchakato huo unalenga kuwapata viongozi wenye sifa, uwezo na dira ya kuendeleza mchezo wa judo nchini, sambamba na kuimarisha uongozi na maendeleo ya chama kwa ujumla.

