KIKAO CHA KAMATI YA UKAGUZI

08 Mar, 2024
Kamati ya Ukaguzi iliyopo chini ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) leo Machi 08, 2024 imekaa na menejimenti ya Baraza kupitia utekelezaji na kujiridhisha na hoja za wakaguzi wa ndani na nje
Aidha kamati imeielekeza menejimenti kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuleta ufanisi.
Kamati hiyo inaongozwa na Mwenyekiti Denis Simba, Katibu George Otieno pamoja na Mjumbe Beatrice Singano.