BMT YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO SHULE YA MSINGI KIBASILA
service image
02 Sep, 2025

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) leo tarehe 2 septemba, 2025 kupitia kwa Afisa michezo mwandamizi Ndg. Charles Maguzu, limekabidhi vifaa vya michezo kwa Bi. Halima Hassan Mwl. Mkuu wa shule ya msingi Kibasila iliyopo katika wilaya Temeke.

Vifaa vilivyotolewa ni Mipira 2 ya soka, 1 wa netiboli, 1 wa wavu, 1 wa kikapu seti 1 ya jezi za soka na pea 1 ya jezi za netiboli, ikiwa ni ahadi ambayo ilitolewa na katibu Mtendaji wa BMT Bi. Neema Msitha alipoalikwa kwenye mahafali ya 59 shuleni hapo yaliyofanyika tarehe 28 Agosti, 2025 jijini Dar es salaam.