BMT WATAKA MAFANIKIO YA NETIBOLI KIMATAIFA

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) wameutaka uongozi wa Chama cha Mchezo wa Netiboli Tanzania (CHANETA) kuhakikisha wanausimamia mchezo huo ili wanamichezo wafanye vema katika mashindano mbalimbali ya kimataifa wanaenda kushindana.
Rai hiyo imetolewa Machi 08, 2022
na Mkuu wa idara ya Rasilimali watu kutoka Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Gerald Mwalekwa huku akiwataka makocha na waamuzi kuitumia elimu waliyoipata kwa maslahi ya Chaneta na timu ya taifa.
"Chaneta wamekuwa na mwanzo mzuri kwenye hili, kama makocha na waamuzi wote 50 watayafanyia kazi yale waliyofundishwa, hakuna shaka Tanzania itapiga hatua kimataifa," alisema Mwalekwa.
Kiongozi huyo pia alimshukuru Filbert Bayi mwenyekiti wa Taasisi za FBF iliyotumika kwa sapoti yake kwenye mafunzo hayo licha ya kwamba hayuko kwenye familia ya netiboli.
"Mzee wetu ni mwanariadha, lakini anatumia rasilimali alizonazo kusaidia maendeleo ya michezo mingine, kwa gharama ambazo mmenieleza amewatoza kwa siku zote mlizoishi katika kituo hiki mkijifunza, na mazingira ya kituo niliyoyashuhudia, sehemu nyingine ingekuwa ni kubwa sana, lakini yeye ameamua kuwasaidia kwa kuwatoza gharama kidogo sana za uendeshaji, mzee wetu huyu azidi kubarikiwa na kuendelea kuwepo kutoa sapoti hii," alieleza.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta), Dk Devotha Marwa amesema mipango ya netiboli kurudi kwenye levo ya kimataifa imeanza kuonyesha matunda.
Alizungumza kuwa kozi hiyo ni kozi ya kwanza ya kimataifa ya netiboli kufanyika nchini na kuwa na muitikio wa
Makocha nane kati ya 26 nchini walioshiriki mafunzo ya kimataifa ya netiboli wametunukiwa vyeti vya Afrika daraja la kwanza.
Makocha hao ni Mussa Samson na Hafidh Tindwa wa Dar es Salaam, Benson George na Frola Odilo wa Dodoma, Everyne Ngonyani, Frola Patrick na Stephen Mzee wa Pwani pamoja na Aneth Kapinga wa Mtwara walitunukiwa vyeti vya Afrika daraja la kwanza ambavyo vinawapa fursa ya kufundisha timu za taifa katika nchi yoyote Afrika.
Makocha wengine wanane waliotunukiwa vyeti vya daraja la dhahabu ambavyo vinawapa fursa ya kufundisha klabu mbalimbali nchini.