BMT YATOA MIEZI MITATU KWA TAWF KUWASILISHA MPANGO WA KULIJENGA SHIRIKISHO
                            
                                
                                     07 Feb, 2023
                                
                            
                            Baraza la Michezo la Taifa BMT kupitia kwa Afisa mwenye dawati la Shirikisho la wanyanyua vitu vizito nchini (TAWF), Nicholas Mihayo ameliagiza Shirikisho hilo kuja na mpango mkakati wa kuimarisha Shirikisho ndani ya kipindi Cha miezi mitatu.
Hayo ameyasema leo Februari 7 2023, katika Kikao na baadhi ya Viongozi wa Shirikisho hilo kilichofanyika katika Ofisi za BMT Jijini Dar es salaam.
Mipango waliyoelekezwa kutekeleza ndani ya miezi hiyo ni pamoja kuandaa uchaguzi mkuu ili kuwapata viongozi wa kuchaguliwa, kusambaza mchezo kwa kuongeza wanachama, kufanya mashindano, kuwa na Ofisi pamoja na kuwa vikao vya majadiliano kwa manufaa ya Shirikisho.

