BMT YAWAAHIDI USHIRIKIANO UMSOTA
service image
26 Oct, 2022

Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo (BMT) Neema Msitha amewaahidi ushirikiano Umoja wa wanasoka wa zamani (UMSOTA) ili kufikia malengo ya kuanzishwa kwa umoja huo.

Msitha ameyasema hayo leo Oktoba 26, 2022 mapema wakati alipofanya nao kikao na kusikiliza hoja na maoni yao tofauti yenye kuujenga umoja wao huku akiwaahidi ushirikiano na kuwataka kufuta taratibu zote katika yale wanayotaka kufanya ili kuimarisha umoja huo.

Kikao hicho kilimhusisha Mtendaji Mkuu wa huyo wa BMT na baadhi ya Maafisa wake pamoja viongozi wa Umsota akiwemo Mwenyekiti Faza Lusozi, Jamal Rwambow, Abbas Kuka (Mjumbe), Rahim Lumelezi (Mjumbe), Isabella Kapera (Mwamuzi, Kamisha mstaafu - FIFA na CAF), Salum Mwinyi (Mjumbe), na Lameck Kibatala (Mjumbe).