UFUNGUZI WA MASHINDANO YA CHAN 2024
service image
30 Jul, 2025

Mwenyekiti wa Kikao cha kamati ya maandalizi ya mashindano ya CHAN 2024 na AFCON 2027 (LOC) Leodigar Tenga, leo tarehe 30 Julai, 2025 ameongoza kikao cha maandalizi ya Mashindano ya CHAN 2024 kilichofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa ,Jijini Dar es salaam.

Lengo la kikao lilikuwa ni kufanya maandalizi ya Mwisho kuelekea ufunguzi wa michuano ya CHAN 2024 yatakayofanyika Tarehe 02 Agosti, 2025 katika Uwanja wa Benjamin William Mkapa kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na Burkinafaso.