KIKAO CHA TATHMINI YA MASHINDANO YA CHAN

04 Sep, 2025
Mwenyekiti wa Kikao cha kamati ya maandalizi ya mashindano ya CHAN 2024 na AFCON 2027 (LOC) Leodigar Tenga, leo tarehe 04 Septemba, 2025 ameongoza kikao cha tathimini ya Mashindano ya CHAN 2024 na maandalizi ya AFCON 2027 kilichofanyika katika Hoteli ya Johari Rotana, Jijini Dar es salaam.
Lengo la kikao hicho ni kufanya tathimini ya Mashindano ya CHAN 2024 kwa kupokea taarifa kutoka kamati mbalimbali zilizoandaa Mashindano hayo yaliyoanza tarehe 02 hadi 30, Agosti, 2025 pamoja na kufanya maandalizi ya mashindano ya AFCON 2027, ambayo Uganda, Kenya na Tanzania bado ni wenyeji wa michuano hiyo.