CHANGALAWE ASHINDA KWA RSC ROUND YA KWANZA NA KUTINGA NUSU FAINALI
service image
20 Mar, 2024

Nahodha wa Timu ya Taifa ya Ngumi "Faru Weusi wa Ngorongor  Yusuf CHANGALAWE ameendeleza wimbi la ushindi kwa Tanzania baada ya kumchakaza mpinzani wake Maxinillano Bibano kutoka Equatorial Guinea katika round ya kwanza tu ya mchezo kwa kwa Mwamuzi kusimamisha pambano yaani *RSC* (Referee stop the contest) baada ya mpinzani huyo kuelemewa na Makonde mazito kutoka kwa Changalawe.

Ni katika bout no. 120 ya uzani wa *Light Heavyweight 80kg* hatua ya robo fainali ambapo Changalawe alitumia Dk 1 tu kumchakaza mpinzani wake na kuibuka na ushindi.

Changalawe amejihakikishia kushinda medali na itakua medali ya 3 kwa Tanzania 🇹🇿 zote zikitokea kwenye mchezo wa Ngumi katika michezo ya Afrika Accra 2023 inayoendelea nchini Ghana.

Mabondia wengine waliofanya hivyo ni Musa Maregesi (Cruiserweight 86kg) na Ezra Paulo Mwanjwango (Lightweight 60kg) ambao wote wako katika hatua za nusu fainali.