CHANGIA TWIGA STAR

01 Mar, 2022
Kuelekee siku ya Wanawake duniani Machi 08, 2022 Serikali kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwa kushirikiana na Taasisi inayojishughulisha na kupinga unyanyasaji wa kijinsia ya Dada Hood wameandaa usiku maalum wa kuchangia Timu ya Taifa ya Wanawake ya mpira wa miguu (Twiga Stars).
Usiku huu maalum utahusisha Viongozi kutoka Serikalini na Taasisi binafsi lakini pia utapambwa na uzinduzi wa album ya 'The Orange Concert' pamoja na wasanii tofauti watakuwepo.
Mafanikio ya 'Twiga Stars' niya watanzania wote kuwa tayari kuunga mkono juhudi za wanawake. Namba za kuchagia zitatolewa muda wowote kuelekea siku hiyo muhimu kwa wanawake.