NAIBU WAZIRI MWINJUMA AHUDHURIA MKUTANO WA 'ANT DOPING' GHANA
service image
07 Mar, 2024

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma ameshiriki mkutano wa kujadili madhara ya matumizi ya dawa za kusisimua misuli michezoni na njia za kukabiliana na madhara hayo leo Machi 7, 2024 jijini Accra Ghana.

Mkutano huo umeandaliwa na Tume ya Umoja wa Afrika ya masuala ya afya ya binadamu na maendeleo ya jamii Idara ya utamaduni na michezo kwa kushirikiana na Wakala wa Kupambana na Dawa za Kusisimua Misuli Michezoni (World Anti Doping Agency - Africa) na kuhudhuriwa na Mawaziri wa Michezo pamoja na wataalamu kutoka takribani nchi 54 zinazoshiriki Mashindano Michezo ya Afrika (All African Games) yanayotarajiwa kuanza Machi 8 hadi 23, 2024 nchini humo.

Kando na Mkutano huo, Naibu Waziri Mwinjuma yupo nchini Ghana kuongoza washiriki kutoka Tanzania katika mashindano ya all African Games ambayo Tanzania inashiriki kwenye michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu upande wa Wanawake chini ya miaka 20, kikapu, kriketi, kuogelea, Judo, baiskeli na riadha.