NAIBU WAZIRI MWINJUMA ASHUHUDIA TIMU YA KUOGELEA IKIPAMBANA

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma Machi 10, 2024, ameshuhudia waogeleaji wa Tanzania Sophia Latiff na Collins Saliboko wakipambana katika mbio za mita 50 za mtindo wa 'butterfly' katika mashindano ya michezo ya Afrika (All African Games) yanayoendelea nchini Ghana.
Sophia alimaliza mbio hizo na kushika nafasi ya 21 kati ya waogeleaji 29 kwa upande wa wanawake na huku Collins akiibuka nafasi ya 16 kati ya waogeleaji 37 kwa upande wa wanaume, wote wawili waliweza kuufikia muda wao waliokuwa nao awali.
Washiriki hao wawili wamebakiwa na michezo miwili miwili ya mita 50 'freestyle' na mita 100 'butterfly' ambapo mchezo mmoja wa mita 100 wa butterfly utachezwa machi 11 na mchezo wa mita 50 freestyle utachezwa Machi 13, 2024.
Naibu Waziri Mwinjuma ameendelea kuona hamasa kwa wachezaji hao na wengine wanaoshiriki michezo mingine kuendelea kupambana ili waweze kuendelea kupeperusha vyema bendera ya Tanzania.
Tanzania ni miongoni mwa nchi 54 zinazoshiriki michezo 29 ya mashindano hayo ikishiriki mchezo wa baiskeli, judo, riadha, mpira wa miguu kwa wanawake chini ya miaka 20 na kriketi wanawake.