NAIBU WAZIRI WA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO MH. HAMISI MWINJUMA ASHIRIKI JOGGING BONANZA
service image
11 Sep, 2023

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Hamis Mwinjuma (Mb) ameshiriki "jogging" kwenye Bonanza la kuadhimisha miaka 9 tangu kuanzishwa kwa Muheza Jogging and Sports Club, ambalo limehudhuriwa na klabu 51 zenye washiriki zaidi ya 683 kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Pamoja na kushiriki mbio hizo, Mhe.Mwinjuma amepata nafasi ya kushuhudia Michezo mbalimbali ikiwemo kuvuta kamba na wanaume kushindana kukuna nazi.

Bonanza hilo limefanyika likiwa na kauli mbiu "Kataa Ukatili wa Kijinsia" ambapo washiriki walipata fursa ya kuelimishwa masuala mbalimbali yanayohusu ukatili wa kijinsia.